Orodha ya wapigakura itawekwa wazi ili wananchi waikague-Waziri Mchengerwa

MWANZA-Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa amesema,orodha ya wapigakura itawekwa wazi ili wananchi waikague.
Ameyasema hayo Oktoba 15,2024 wakati akizungumza na vyombo vya habari jijini Mwanza kufafanua hoja mbalimbali zilizoibuliwa na wadau wa uchaguzi hususani ni kipindi hiki cha uandikishaji.

"Baadhi vyama vimekuwa vikitaka kupata takwimu za uandikishaji kila siku kutoka kwa waandikishaji.

"Nitoe ufafanuzi juu ya jambo hili ni kwamba mawakala wanatekeleze jukumu lao la msingi la kuhakikisha wananchi wanaofika kujiandikisha wanajindikisha kwa mujibu wa kanuni namiongozo pasipo bugudha.

"Suala la ukaguzi wa Daftari hilo lipo kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi. Kanuni ya 10 (4) na (5), Tangazo la Serikali Na.572 na Kanuni ya 11(4) na(5) Tangazo la Serikali Na.571,573 na 574 zimeweka wazi kuwa baada ya zoezi kukamilika orodha ya wapigakura itabandikwa na wananchi wote wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa watakagua daftari ili kujiridhisha na usahihi wa orodha iliyoandaliwa.

"Endapo kutakuwa na kasoro yoyote itakuwa ni fursa ya kurekebisha kasoro hizo. Kwa sasa Waandikishaji wapewe nafasi ili watekeleze jukumu hilo kwa mujibu wa kanuni.

"Msimamizi msaidizi wa uchaguzi atabandika kwenye mbao za matangazo ya Uchaguzi orodha ya wapigakura ili wananchi waweze kukagua orodha hiyo kuanzia Oktoba 21 hadi 27,2024.

"Endapo kutakuwa na changamoto zinazohitaji kuchukua hatua za haraka, wapo wasimamizi wasaidizi, au wasimamizi wa uchaguzi hivyo muwasilishe changamoto kwenye mamlaka husika ili iweze kuzichukulia hatua."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news