Pamba Jiji FC yavunja mkataba na makocha wake

MWANZA-Klabu ya Pamba Jiji FC imethibitisha kufikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu Goran Kopunovic pamoja na kusitisha mikataba ya wasaidizi wake, Salvatory Edward, Kocha wa magolikipa Razack Siwa na kocha wa viungo Cirus Kakooza.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Oktoba 16, 2024 iliyotolewa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Ezekiel Ntibikeha ikibainisha kuwa, kwa sasa timu itakuwa chini ya Kocha Mathias Wandida aliyekuwa kocha wao wa U-20 hadi hapo atakapotangazwa kocha mkuu.

“Uongozi unawashukuru kwa muda wao wote waliokuwepo hapa klabuni na unawatakia kila la kheri katika maisha yao nje ya Pamba Jiji;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news