Rais Dkt.Mwinyi ajumuika na wananchi Kisiwa cha Tumbatu

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi, amejumuika na waumini wa dini ya Kiislamu huko Tumbatu, Jongowe katika maadhimisho ya Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW).
Alhaj Dkt. Mwinyi aliambatana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa, na Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Haroun Ali Suleiman, Mhe. Haji Omar Heri Mwakilishi wa Jimbo la Tumbatu.
Oktoba 1, 2024 alipowasili Tumbatu alipokelewa na viongozi wa Dini, Serikali, Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama, na mamia ya wananchi wa Tumbatu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news