ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameshiriki kikao cha Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Oktoba 25, 2024 Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar.
Kikao hicho kimeongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.