DOHA-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akiendelea na ziara yake Doha,Qatar ametembelea kituo kikubwa cha kujitolea cha Qatar kinachojishughulisha na kutoa misaada kwa wenye mahitaji mbalimbali cha Qatar Charity na kujionea shughuli zinazofanywa na kituo hicho.

Amefurahishwa zaidi kuona idadi kubwa ya misaada inayotolewa na kituo hicho.
Miongoni mwa nchi zinazonufaika na kazi kubwa inayofanywa na Qatar Charity ni pamoja na Tanzania ambapo wanayo ofisi yao Dar es Salaam.
Rais Dkt.Mwinyi ameonesha matumaini yake kwa kituo hicho na kuwataka kupanua zaidi shughuli zake maeneo mengine ya Tanzania.