ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amehudhuria msiba wa aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba marehemu, Bi. Thereza Olban Ali, nyumbani kwake Miembeni, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Rais Dkt. Mwinyi ametoa salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa, na marafiki leo Oktoba 15,2024.

Halikadhalika, aliwahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba mwaka 1983 na alihudumu katika nyadhifa mbalimbali ndani ya CCM na Jumuiya zake.