Rais Dkt.Mwinyi atoa wito kwa taasisi za elimu ya juu nchini

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amezishauri taasisi za elimu ya juu zilizo nchini kuanzisha kozi muhimu zenye uhitaji na uhaba wa wataalamu, ambazo zitachangia maendeleo ya nchi.
Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa hatua hiyo itasaidia sekta ya afya kuwa na wataalamu wa kutosha katika kada mbalimbali, watakaotoa huduma kwa kuzingatia utaalamu na weledi, hivyo kuimarisha sekta ya afya.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo kwenye mahafali ya 12 ya Zanzibar School of Health leo, OOktoba 19,2024 katika viwanja vya Mao Tse Tung, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Rais Dkt. Mwinyi ametoa wito kwa wahitimu wa kada tofauti wazingatie nidhamu na maadili ya kazi katika utoaji wa huduma wanapoingia kwenye majukumu yao, na kuwa msaada muhimu kwa jamii.

Aidha, amewasisitiza vijana kusoma kozi zenye umuhimu na uhitaji, hususan zinazoanzishwa na Zanzibar School of Health, huku akiipongeza juhudi zinazochukuliwa na chuo hicho kuanzisha kozi mpya.

Halikadhalika Rais Dkt. Mwinyi amefafanua kuwa juhudi hizo zinaendana na malengo ya Serikali ya kuhakikisha chuo hicho kinakuwa chemchem ya kuzalisha wataalamu katika sekta ya afya.
Vilevile, ametoa wito kwa wahitimu wa chuo hicho kujiendeleza zaidi kielimu pale fursa zinapojitokeza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news