Rais Dkt.Mwinyi awasili Mwanza

MWANZA-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameondoka Zanzibar na kuwasili Mwanza kuhudhuria Kilele cha Mwenge wa Uhuru na kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kitakachofanyika kesho mkoani humo.
Katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza , Dkt. Mwinyi amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali , Chama Cha Mapinduzi, pamoja na Vyombo vya ulinzi na usalama.
Akiwa mkoani humo, Rais Dkt. Mwinyi leo Oktoba 13,2024 atazindua tawi la Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) lililopo jijini Mwanza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news