ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewasili Pemba kushiriki maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani.

Dkt. Mwinyi atakuwa Mgeni Rasmi kwenye kilele cha maadhimisho ya siku wa Wazee duniani ambayo kwa Zanzibar yanaadhimishwa viwanja vya Tibirinzi, Wilaya ya Chake chake, Mkoa wa Kusini Pemba, leo tarehe 07 Oktoba, 2024.