ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkr. Hussein Ali Mwinyi, amewasili kisiwani Pemba kuendelea na shamrashamra za mafanikio ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Nane madarakani.
Katika Uwanja wa Ndege wa Pemba, Rais Dkt. Mwinyi amepokelewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, pamoja na viongozi wa Serikali, Chama Cha Mapinduzi, na vyombo vya ulinzi na usalama.
Rais Dkt. Mwinyi atafungua Skuli ya Konde Sekondari na kushiriki kilele cha kampeni ya "Kijana na Kijani," kilichoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi katika Uwanja wa Gombani, Pemba.
31 OKTOBA, 2024