Rais Dkt.Mwinyi azidisha tabasamu kwa wazee Zanzibar

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameiagiza Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi kuishughulikia Sheria ya Vyombo vya Barabarani na kuharakisha mchakato wa kuwapatia wazee vitambulisho maalumu vitakavyowasaidia kulipa nusu nauli kama ilivyo kwa wanafunzi na watu wenye ulemavu.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema Oktoba 7,2024 kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani katika Ukumbi wa ZSSF, Tibirinzi Wilaya ya Chake Chake, Mkoa wa Kusini Pemba.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ameziagiza taasisi zote za Serikali, zinazotoa huduma za usatawi kwa Wazee, kuzishughulika haraka na kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili wazee hao.
Taasisi zilizopewa maagizo hayo ni Wizara ya Afya kuagizwa kuandaa madirisha maalumu hospitali zote kutoa huduma bora za Wazee kwa kuwapa kipaumbele, pamoja na kuongeza madaktari bingwa wa magonjwa ya wazee.

Halikadhalika, Wizara ya Fedha imeagizwa kuandaa bajeti maalumu ya kuendesha mabaraza ya wazee pamoja na kufungua madirisha maalumu kwenye benki na vituo vyote vinavyotoa huduma za Fedha kuwapa kipaumbele wazee hao.
Rais Dkt. Mwinyi amesema, Serikali imeandaa na inaendelea kutekeleza Sera ya Hifadhi ya Jamii ya mwaka 2014 ambayo imeweka mikakati madhubuti ya kusimamia maendeleo ya wazee.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news