DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Abbot,Bw. Robert Ford pamoja na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 3 Oktoba, 2024.
Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan akiteta na ujumbe kutoka Abbott Fund ulipofika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Abbot,Bw. Robert Ford akiwa katika mazungumzo hayo.
Mfuko wa Abbott ulianzishwa na Abbott mwaka 1951 kama msingi wa hisani huku ukiwekeza katika mawazo mapya yanayopanua ufikiaji wa huduma za afya, kuimarisha jumuiya mbalimbali kwa kufanya kazi na kukuza elimu ya sayansi na afya.