MOROGORO-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa ruzuku ya bei kwenye mitungi ya gesi inayotolewa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ili Watanzania watumie nishati safi na salama kwa afya zao pamoja na kuhifadhi mazingira nchini.



Ameongeza kuwa, REA wameanza kutoa majiko banifu 790 kwa wananchi wa Gairo ambayo ni majiko rafiki, imara REAukwa muda mrefu, yanatunza mazingira na yanatumia kiasi kidogo cha mkaa.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabir Makame amemshukuru Rais Samia kwa kutoa ruzuku ya bei kwenye mitungi hiyo kwa wananchi wake ambapo itarahisisha upatikanaji wake kwa wingi.
"Wananchi wenzangu wa Gairo, majiko haya ni rafiki kwa matumzi, salama kwa afya zenu, ni msaada mkubwa katika utunzaji na uhifadhi wa mazingira yetu. Nawahimiza kuyanunua ili nishati hii iwe na manufaa makubwa kwenye familia zetu badala ya kuendelea kukata miti kupata mkaa na kuni, "amesema Mhe. Makame
Tags
Habari
Nishati Safi ya Kupikia kwa Wote
REA Tanzania
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Wizara ya Nishati Tanzania