Rais Dkt.Samia ana matumaini makubwa na Taifa Stars-Waziri Mkuu

DAR-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitembelea Timu ya Taifa ya Tanzania ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) inayofanya mazoezi kwenye uwanja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) jijini Dar es Salaam na kusema kuwa, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anamatumaini makubwa kuwa timu hiyo itafanya vizuri kwenye michezo yote miwili.Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo Jumatatu, Oktoba 07, 2024 alipozungumza na wachezaji, benchi la ufundi pamoja na viongozi wakiwa katika maandalizi ya michezo miwili ya kufuzu michuano ya AFCON 2025 dhidi ya Congo itakayochezwa Oktoba 10 na 15, 2024.
“Kila mmoja aone ana jukumu kubwa, kwako wewe mwenyewe na kwa nchi yako, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia anawatakia kila la kheri na alichofanya ametoa usafiri wa uhakika wa ndege itakayowapeleka nchini Congo kwa ajili ya mchezo wa Oktoba 10, 2024, hili ni jambo kubwa.”

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa kwa jitihada za Rais Dkt. Samia amefanikiwa kushawishi mashirikisho ya mpira wa miguu ya Afrika na FIFA ili kuiona Tanzania ni nchi ambayo imeamua kuboresha viwango vya michezo ikiwemo mpira wa miguu.
“Tumeanza kuona heshima tunayoipata ya kuwa wenyeji wa baadhi ya mashindano ikiwemo CHAN.”

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amewataka wachezaji hao kushikamana, kuzungumza lugha moja na kutanguliza uzalendo.

“Tumieni fursa ya imani ya Watanzania kwenu kuiwakilisha vyema Tanzania kwenye michezo iliyo mbele yenu.”
Kwa upande wake, Nahodha wa timu hiyo Mohammed Hussein “Tshabalala” amemshukuru Rais Dkt. Samia kwa kuwezesha kupatikana kwa usafiri wa ndege kwa ajili ya mchezo dhidi ya Congo. 

“Kwetu sisi hii ni motisha kuelekea michezo yetu miwili dhidi ya Congo, kwasababu itatusaidia kurejea haraka nyumbani kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news