Rais Dkt.Samia apambania Mfuko wa Taifa wa Maji (NWF)

DAR-Mfuko wa Taifa wa Maji (NWF) unafanikisha ujenzi wa miradi ya maji katika maeneo yenye uhitaji mkubwa hapa nchini.NWF inalo jukumu la msingi la kutafuta fedha za utekelezaji wa miradi ya maji, mjini na vijijini ambapo Serikali ya awamu ya sita inahakikisha jambo hilo linafanikiwa kwa wananchi kufikiwa na huduma ya majisafi.

Mtendaji Mkuu wa NWF, Wakili Haji Nandule amesema hayo leo Oktoba 31,2024 jijini Dar es Salaam katika kikao kazi na wahariri na waandishi wa vyombo vya habari chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR).

Amesisitiza kuwa, Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanikisha upatikanaji na matumizi ya fedha ambapo asilimia 60 ya fedha hizo zinapelekwa katika kufanikisha miradi ya maji vijijini kupitia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA).
Amesema, NWF imefungua Dirisha la Mkopo Wenye Masharti Nafuu mahsusi katika kutekeleza miradi ya maji kwa mamlaka za maji hapa nchini na tangu mwezi Julai 2024 kiasi cha shilingi bilioni 5.3 kimetolewa kama mkopo kwa mamlaka za maji za Tanga UWASA, Bunda na Dar es salaam (DAWASA).

Mwenyekiti wa Bodi ya NWF, Mhandisi Abdallah Mkufunzi amesema, taratibu za kutoa mkopo hiyo zinapitiwa zaidi ili kuweza kuimarisha ujenzi wa miradi ya maji na uendelevu wake kwa faida ya wananchi.

Naye Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Bw. Prosper Buchafwe amesema Serikali inao mgawanyo wa majukumu na kila taasisi ya Wizara ya Maji inalo jukumu lake la msingi, NWF ikiwa na kazi ya kutafuta fedha, wakati mamlaka za maji zikiwa na jukumu la msingi la kutoa huduma maji kwa wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news