DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa ridhaa ya kuanza mchakato wa kutengeneza Arena katika viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam, ambapo shughuli za sanaa na burudani zitafanyika.


“Huko tunapoelekea, hamtakuwa mnatumia nguvu nyingi kuwaleta watu kushuhudia stand-up comedy. Mhe. Rais ameshatupa ruhusa hii, na mchakato umeshaanza. Kile kilio chenu cha kupata sehemu mahsusi kwa ajili ya shughuli hii, Mhe. Rais amekisikia na ameshatupa ruhusa ya kukifanyia kazi,” alisema Mhe. Mwinjuma.
Tukio hili, ambalo ni mara ya kwanza kufanyika kwenye viwanja hivyo na kukusanya umati wa watu, pia limehudhuriwa na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete, ametoa pongezi kwa CHEKA TU kwa kutimiza miaka saba na mafanikio ambayo wameyapata mpaka sasa.