Rais Dkt.Samia ashiriki kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na Kumbukizi ya Miaka 25 ya Kifo cha Baba wa Taifa

MWANZA-Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 kimefanyika leo, Oktoba 14, 2024, katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye alikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Kiongozi wa Mbio za mwaka huu, Godfrey Mzava.
Mbio hizi pia zimeambatana na kumbukizi ya miaka 25 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Tukio hilo ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa, ambayo imeanza Oktoba 8, 2024, na ilijumuisha shughuli mbalimbali kama kongamano la fursa za ujasiriamali kwa vijana na maonesho ya bunifu za vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news