Rais Dkt.Samia ateta na ujumbe kutoka Vodacom Group

DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kundi la Makampuni ya Vodacom, Bw. Sakumzi Macozoma pamoja na ujumbe wake mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 03 Oktoba, 2024.
Vodacom ni miongoni mwa kampuni za mawasiliano duniani ambazo zimeendelea kuwa na mchango mkubwa zaidi kwa jamii mbalimbali, kwa hapa nchini Vodacom Tanzania imekuwa ikiwezesha mawasiliano ya simu kwa wananchi, huduma za intaneti.
Vilevile imeendelea kuonesha umahiri mkubwa katika utoaji wa huduma za kifedha zisizo za kibenki ambapo kutokana na mtandao kuwa na uwanda mpana wa mawasiliano, si mijini tu wananchi wanafurahia mawasiliano ya simu na huduma za kutoa na kutuma fedha, vivyo hivyo katika vijiji mbalimbali.
Kundi hilo la makampuni limepanua huduma zake Tanzania, Afrika Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Misri, Ethiopia, Kenya, Lesotho, Msumbiji na kwingineko.

Vodacom inamilikiwa na Vodafone kwa hisa asilimia 65, ikiwa moja ya kampuni kubwa zaidi za mawasiliano duniani kwa mapato.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news