MWANZA-Ziara ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan mkoani Mwanza imeanza siku ya leo na kwa umuhimu mkubwa katika kuimarisha maendeleo ya mkoa huo, pia inatarajiwa kutoa fursa kwa wananchi kuwasilisha changamoto wanazokabiliana nazo moja kwa moja.

Sambamba na kutoa maelekezo mahsusi ya kuharakisha utekelezaji wa miradi hiyo ili kufikia malengo ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Aidha, ziara hii itakuwa jukwaa muhimu kwa Rais Dkt.Samia kuzungumza na wananchi, kuhamasisha ushirikiano wa karibu kati ya serikali na jamii katika kukuza uchumi wa viwanda, pamoja na kuboresha huduma za kijamii.
Hali kadhalika, hotuba zake zinatarajiwa kugusia masuala ya kisera, akisisitiza umuhimu wa utulivu na amani kama nguzo za msingi katika safari ya maendeleo ya taifa.