Rais Samia ametutendea wema wananchi wa Isimani-Waziri Lukuvi

IRINGA-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani amemushukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi barabara kwa kiwango cha lami kutoka Kijiji cha Msembe lango la Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mpaka Iringa Mjini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani akizungumza na wananchi wa kijiji cha Idodi, Tungamalenga, na Mapogoro katika mikutano ya hadhara aliyofanya katika kata ya Idodi.

Waziri ametoa shukrani hizo wakati wa ziara yake katika kata ya Idodi ya kutembelea miradi ya maendeleo ambapo pia amepata fursa ya kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika kitongoji cha Msimbi kilichopo katika kijiji cha Idodi leo tarehe 20/10/2024.

Amefafanua kwamba, ujenzi wa barabara hiyo ni shauku ya watu wa Jimbo la Isimani waliyokuwa nayo kwa muda mrefu na kampuni ya Chicco ndio imeshinda tenda ya ujenzi wa kipande hicho cha barabara.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani akizungumza jambo na Afisa Mipango wa Halmashauri ya Iringa Bw. Exavery Luyagaza katika ziara yake kata ya Idodi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani akizungumza na wananchi wa kijiji cha Idodi, Tungamalenga, na Mapogoro katika mikutano ya hadhara aliyofanya katika kata ya Idodi.

"Barabara hiyo itaajiri Watanzania kwa shughuli watakazoweza kufanya na Miji yetu Mikubwa ya Tungamalenga, Idodi, na Mapogoro itawekwa taa za barabarani.”

Aidha,kwa upande wa Isimani Serikali imejenga miuundo Mbinu ya maji na kusaidia wananchi wa Tarafa ya Isimani kupata maji safi, kwa kutoa Maji kutoka Kilolo na Kuleta Isimani na kuchukua Maji kutoa Iringa Mjini na Kuleta Isimani hivyo kila kijiji kinapata huduma ya maji safi na salama.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani akisalimiana na watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo katika kata ya Idodi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu), Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani akifurahi burudani ya muziki kutoka kwa vijana wa kitisi wakati alipofanya Mkutano wa hadhara katika kijiji hicho.

Waziri Lukuvi amesema katika eneo la Pawaga Serikali imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa mfereji mkubwa wa umwagiliaji na hivyo kusaidia mashamba makubwa ya umwagiliaji katika eneo hilo kwa kusaidia shughuli za kilimo na kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi.

“Mhe. Rais, Dkt Samia Suluhu Hassani ametufanyia wema mkubwa watu wa Isimani kwa kutimiza shauku ya kupata mambo tuliyokuwa tunahitaji katika kipindi chake kifupi cha miaka mitatu," alisema.
Kwa upande wake Diwani wa Idodi, Mhe. Julius Mbuta amesema anaishukuru serikali kwa kuleta fedha nyingi za miradi ya maendeleo katika kata ya Idodi, na kuondoa changamoto za upatikanaji wa maji safi na salama.

“Ukarabati wa miundo mbinu ya barabara umesaidia maeneo mengi katika kata ya Idodi kufikika kirahisi hivyo kusaidia wananchi kurahisisha mawasiliano kutoka eneo moja kwenda eneo jingine,”alisema Mbuta.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news