NA LWAGA MWAMBANDE
LEO pia, msomaji wangu ninakusogezea diwani nyingine ya SADAKA INA HARUFU, ikiwa ni kitabu cha tatu kati ya vile vitano ambavyo nilivizindua Oktoba 17,2024 kupitia Moto Ulao Online Church (MUOC).
Diwani ya SADAKA INA HARUFU ni matunda ya mafundisho yanayotolewa na Mchungaji Imani Oscar Katana wa Moto Ulao Online Church (MUOC). Anatoa mafundisho kupitia mitandao ya kijamii kama WhatsApp, Facebook na YouTube.
Diwani hii imegawanyika katika sehemu tatu.
i. Mashairi yanayohusu sadaka, yenye kichwa kinachosema Toa upate kutoka na kwamba kila kitu unachokitoa ni sadaka ambayo majibu yake (Malaki 3:10-12). Moja ya beti katika sehemu hii inasema:
Sadaka ina harufu, iko mbaya iko nzuri,
Ya kuleta utukufu, hiyo usiihariri,
Na nyingine ya kukifu, Kaini ni yake mbari,
Ni vipi sadaka yako, yanukia inanuka?
ii. Mashairi yanayohusu umuhimu wa watu wanaojitoa kwako na kukuletea furaha, amani, na mafanikio, na inaitwa Kuna watu manukato.
Ukisoma na kuimba mashairi haya utapata nafasi ya kumshukuru Mungu kama unao watu kama hao pamoja na kuwaombea. Nawe utajitathmini kama ni kivuli au manukato kwa wengine na kisha utachukua hatua stahiki.
SOMA:Cheza na ahadi zako
Kuna watu manukato, vizuri wananukia,
Ni miti yenye mvuto, kila mtu awania,
Kuwa nao ni kipato, maisha tafurahia,
Muumba akujalie, pata watu kama hao.
iii. Mashairi yanaeleza kwamba Mungu anafanya kitu, sisi tukifanya kitu. Tujitahidi kuwa na kitu ili Mungu afanye kitu kwetu. Ndivyo ilivyokuwa kwa Ibrahimu, kwa mwanamke wa Sarepta, kwa Musa, kwa Dorkasi na wengine wengi:
Wa tano tano kaleta, mbili mbili twaziona,
Wa moja yeye kagota, kuzalisha hakuona,
Mungu anafanya kitu, sisi tukifanya kitu.
Bofya hapa kusoma kurasa zote 34>>>