Serikali imeweka uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya afya-Rais Dk.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali amesema Serikali imeweka uwekezaji mkubwa wa miundombinu ya Afya kutokana na umuhimu wa sekta hiyo kwa jamii.
Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo leo Oktoba 15, 2024 Ikulu jijini Zanzibar alipozungumza na Meneja Mwandamizi wa Mfuko wa Dunia (Global Fund), Dkt. Sara Asiimwe na ujumbe wake ulioongozwa na Waziri wa Afya, Nassor Ahmed Mazrui.
Aidha Rais Dkt.Mwinyi ameishukuru Global Fund kwa jitihada zake za kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuisaidia kwenye masuala mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo Sekta ya Afya.
Halikadhalika, Rais Dkt. Mwinyi ameeleza juhudi za Global Fund kuisaidia Zanzibar kwenye sekta ya Afya na nyengine za maendeleo ni kuendeleza jitihada za Serikali anayoiongoza katika kutekeleza adhma ya Serikali kutoa huduma bora za afya.
Akizungumzia huduma ya bima ya Afya kwa wageni wanaoingia Zanzibar, Rais Dkt. Mwinyi, ameieleza Global Fund dhamira ya Serikali kuja na bima hiyo kutokana na umuhimu wake kwa wageni, hivyo ameuomba Mfuko huo kuangalia namna ya kuiungamkono Serikali.
Naye, Dkt. Sara Asiimwe alimueleza Rais Dk. Mwinyi kwamba Global Fund inafanya kazi kwa karibu zaidi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Sekta zake za Maendeleo ikiwemo Wizara ya Afya. 
Aidha, aliiahidi Serikali kwamba taasisi yao itaendeleza ushirikiano wake na Zanzibar hasa kwenye miradi ya maendeleo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news