Serikali itaendelea kuthamini mchango wa vyama vya siasa katika kudumisha amani-Waziri Lukuvi

DAR-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe William Lukuvi amesema Serikali itaendelea kuheshimu misingi iliyowekwa na vyama vya siasa katika kujenga amani na utulivu kwa watanzania wote.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi akipokea tuzo kwa Kudumisha Umoja na Mshikamano ndani ya Vyama vya Siasa na kuishi 4R za Mhe, Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassani kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha (UDP) Mhe. John Cheyo.

Kauli hiyo ameitoa Oktoba 8,2024 jijini Dar es Salaam katika ziara yake ya kutembelea Makao Makuu ya Ofisi za Vyama vya UDP, NCCR MAGEUZI, CUF na NLD ambapo amepata nafasi ya kukutana na kufanya mazungumzo na Viongozi Wakuu wa Vyama hivyo.
Ameeleza kwamba, tangu mfumo wa vyama vingi umeanza nchini Vyama vya Siasa kwa kushirikiana na Chama Tawala vimekuwa mhimili wa kujenga amani na umoja, hivyo nawapongeza kwa kazi nzuri ya uzalendo mnayofanya.
Katibu wa Chama (NLD) Ndg, Doyo Hassan Doyo akizungumza wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe William Lukuvi na Msajili wa Vyama Vya Siasa Jaji Fransis Mutungi walipotembelea Makao Makuu ya chama hicho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu),Mhe. William Lukuvi akimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi Joseph Selasini alipotembelea Makao Makuu ya chama hicho Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa chama cha (UDP), Mhe. John Cheyo akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi na Msajili wa Vyama Vya Siasa Jaji. Fransis Mutungi walipotembelea Makao Makuu ya Chama cha UDP.

“Niombe Viongozi wa Vyama mhimize wananchi kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha ndani ya demokrasia ya vyama mnaweka wagombea ili washindane na vyama vingine kupata viongozi,” amesema Waziri Lukuvi.

Aidha,Serikali itahakikisha matangazo yote ya vijiji yanawekwa kwenye tovouti za Serikali ili wananchi wafahamu vijiji, vitongoji na mitaa inayogombaniwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi na Msajili wa Vyama Vya Siasa Jaji. Fransis Mutungi wakisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha (NLD) Ndg, Mfaume KHamis na Katibu Wake Ndg, Doyo Hassan Doyo katika Makao Makuu ya chama hicho.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha (UDP),Mhe. John Cheyo amemshukuru Waziri wa Nchi kwa kufanya ziara katika Ofisi za Makao Makuu ya Vyama kwa sababu imeonesha dhamira ya dhati ya Serikali katika kutekeleza falsafa ya 4R.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe William Lukuvi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chama cha (CUF) mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo katika Makao Makuu ya Chama hicho.

"Sisi kama wadau wa siasa tunataka kushiriki katika kuona nchi inatawalika kwa amani na kuchagiza maendeleo makubwa.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news