NA DIRAMAKINI
SERIKALI inatarajia kuzindua vitambulisho vya Kidigitali kwa Wamachinga kesho Oktoba 17,2024 mkoani Arusha ili vianze kusambazwa kwa walengwa kwa ajili ya kuwawezesha kufikia fursa mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Oktoba 16,2024 kwa wanahabari na Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mheshimiwa Dkt.Dorothy Gwajima (Mb);