Serikali yafungua shamba la Othman Khamis Ame kuwezesha huduma za ujenzi

ZANZIBAR-Wizara ya Maji, Nishati na Madini imelifungua shamba la ndugu Othman Khamis Ame lilopo Donge Mchangani Wilaya ya Kaskazini A Unguja kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali za miradi ya ujenzi.
Waziri wa Maji, Nishati na Madini, Mhe. Shaibu Hassan Kaduara ameyasema hayo Oktoba 2,2024 wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari katika ukumbi wa Wizara hiyo Maisara.

Amesema,wananchi wanapaswa kutambua kuwa, Serikali haikufanya mabadiliko yoyote ya bei za maliasili zisizorejesheka.

"Kumekuwa na tabia ya baadhi ya madereva kusingizia ugumu wa upatikanaji wa vibali na kuwalangua wananchi,"amesema Waziri Kaduara.

Pia, amesema Serikali inaendelea kuzuia matumizi na usafirishaji wa mawe katika shughuli za ujenzi na kuvitaka viwanda vinavyojishughulisha na uzalishaji wa kokoto kufanya shughuli zake katika maeneo yenye mawe ili kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.

Amesema, Serikali kwa kuona uharibifu mkubwa wa mazingira pamoja na malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya athari wanazozipata kutokana na uwepo wa viwanda vya kusagia mawe karibu na makaazi ya wananchi,Serikali imeamua kuchuku uamuzi huo.

Pia,amewashauri wananchi kubadilisha utamaduni wa ujenzi na kutumia tofali badala ya mawe kama ilivyo katika mikoa mingine ya Tanzania Bara.

Hatua hiyo imekuja baada ya kufungwa kwa shamba la ndugu Azizi Khamis Azizi liliopo Donge Muwanda Wilaya ya Kaskazini A Unguja kutokana na kumalizika kwa mchanga unaofaa kwa shughuli za ujenzi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news