KILIMANJARO-Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kusogeza huduma za Afya karibu na wananchi kwa kujenga vituo vya Afya Vitano katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.

"Mkoa huu wa Kilimanjaro umepokea zaidi ya Bilioni 10 ili kutekeleza miradi ya Afya vilevile Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongeza milioni 150 kwa ajiri ya vifaa tiba vitakavyotumika katika kituo cha Afya Masama Kati."

"Kwa kuwa Mhe. Rais Samia ameleta Milioni 100 ya umaliziaji wa Zahanati hii na Milioni 50 ya ununuzi wa vifaa tiba, jambo la kwanza naomba fedha ya vifaa ipelekwe Bohari ya Dawa haraka sana, nimachotaka kuona Zahanati hii upatikanaji wa dawa usiwe wa mashaka."
Waziri Mhagama ameukata uongozi huo kuhakikisha huduma za uzazi wa dharula kwa kina mama zinapatikana ikiwemo vitanda maalum vya kujifungulia ili wakina mama wapate eneo salama na zuri la kujifungua na kuwapunguzia adha wananchi ya kufuata huduma hizo mbali.
"Tunatamani Zahanati hii iwe mkombozi kwa akina mama, wazee, vijana na watoto wetu, nitoe wito kwa Halmashauri yetu kuhakikisha Zahanati yetu inasimamiwa vizuri na tunaamini Zahanati hii itaenda kutoa huduma zinzotakiwa."