DAR-Serikali kupitia Wizara ya Fedha imebadilishana uzoefu na Washirika wa Maendeleo kuhusu ushirikiano kati ya Serikali na washirika wa maendeleo, mchakato wa bajeti ya Serikali pamoja na Mwongozo wa Usimamizi wa Miradi na Majadiliano ya Mikopo, Dhamana na Misaada katika Semina ya Ushirikiano kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo nchini.
Semina hiyo iliyofanyika katika Ofisi za Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) jijini Dar es Salaam imeongozwa na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Madeni kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Omary Khama kwa upande wa Serikali na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), Bw. Mark Bryan Schreiner, kwa upande wa Washirika wa Maendeleo.