Serikali yasaini makubaliano na AUDA NEPAD maeneo matano Sekta ya Afya

DAR-Serikali kupitia Wizara ya Afya na Wakala wa Maendeleo wa Umoja wa Afrika (AUDA NEPAD) wamesaini makubaliano ya ushirikiano kwenye maeneo matano ya afya ikiwa ni pamoja na kuboresha afya ya uzazi huku Bima ya Afya kwa Wote ikiwa ni moja ya mambo yatakayoshugulikiwa. Makubaliano hayo yamesainiwa tarahe 19 Oktoba, 2024 ofisi ndogo za Wizara ya Afya, jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amesema AUDA NEPAD wako tayari kutoa kiasi cha Dola Milioni Moja (Tsh: bilioni 2.8), zitakazotumika kwenye maeneo ya ushirikiano.

Waziri Mhagama ameeleza kuwa ushirikiano huo pia utawezesha kuwa na wahudumu wa afya ngazi ya jamii wawili kwa kila mitaa, ambao watasaidia kupambana na magonjwa ya milipuko na kupima magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza.
Ameongeza kuwa,mpaka sasa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imeshapata kiasi cha Dola Laki Tatu kwa ajili ya usimamizi wa kutosha wa usalama wa vifaa vya afya.

"Tunataka kuweka mifumo zaidi ya kusimamia vifaa vya afya na tutahakikisha kwamba malengo yanafikiwa na tukifanya vizuri bidhaa za afya hazitakuwa na maswali," amefafanua Waziri Mhagama.
Waziri Mhagama amesema eneo lingine ni la afya ya uzazi kwa vijana waliopo shule za sekondari ambapo wamepanga kusaidia ili kuepuka mimba zisizotarajiwa kwa vijana hao na kuboresha vituo vya afya ya uzazi, ili kuokoa maisha ya watoto wachanga.

"Vilevile, tumekubaliana kwa pamoja kupambana na unyanyasaji wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto na kutumia akili mnemba katika Sekta ya Afya, hali itakayosaidia wataalamu kushirikiana kwa haraka na minyororo mingi kama dawa, tiba na mengine kufikika kwa urahisi," amesema Waziri Mhagana.
Waziri Mhagama ameishukuru AUDA NEPAD ambayo imeiunga mkono Tanzania katika maeneo hayo makubwa matano ya Sekta ya Afya.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji MKuu wa AUDA NEPAD Bi. Nardos Bekele amesema, wametenga kiasi cha Dola Milioni 100 kwa ajili ya miradi mbalimbali kwenye nchi za Afrika.

"Tunayo furaha tuko hapa kushirikiana nanyi tunaunga mkono mnachofanya, hii itawezesha kukuza uchumi wa Afrika, hivyo kwa pamoja tunahakikisha kuwa jitihada zinazofanywa zinaungwa mkono na kuzaa matunda," amesema Bi. Bekele na kuongeza kuwa AUDA NEPAD itaendelea kuwekeza Tanzania na itaongeza fedha zaidi kama utekelezaji utakuwa ni mzuri.
Aidha,Bi. Bekele ametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na mambo mengi mazuri anayoyafanya chini ya uongozi wake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news