Siku 100 za kuhudumu kama Kamishna Mkuu wa TRA

NA CPA YUSUPH MWENDA

Namshukuru Mungu kwa kibali cha kutimiza siku 100, nikiwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA), baada ya kuaminiwa na Kuapishwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Namshukuru sana Mhe. Rais, kuendelea kuniamini kumsaidia kusimamia uendeshaji wa TRA.

Pia Nawashukuru viongozi wote wa Serikali, Wananchi na Walipakodi wote, Mwenyekiti na Bodi ya Wakurugenzi ya TRA, Pamoja na Watumishi Wote wa TRA kwa Ushirikiano mkubwa wanaonipa.

Katika kipindi cha siku 100, Kwa pamoja tumethibitisha kwamba;

1. Tunaweza kuwa na Ushirikiano na Uhusiano mzuri kati ya TRA na Walipakodi bila ya Kuhatarisha Ulipaji Kodi Stahiki Kwa mujibu wa sheria kama tulivyofanya.

2. Tunaweza Kuongeza Makusanyo ya Kodi bila ya Migogoro na Walipakodi, kama ilivyowezekana ktk Makusanyo ya robo mwaka ya kwanza ya ( Julai - Sept, 2024) kwa kuongeza asilimia 18 ya makusanyo ya kodi.

3. Tunaweza Kuwatembelea na Kuwasikiliza Walipakodi wa nchi nzima (kama tulivyotembelea Mikoa 25 nchi nzima) ili Kuwasikiliza, Kutatua Migogoro yao ya Kikodi kwa wakati pamoja na kuwa Wabunifu wa kutumia mifumo rahisi ya Kuwasikiliza ili kupata mrejesho toka kwa wananchi na walipakodi Wote.

4. Tunaweza kuwekeza na kuharakisha ujenzi wa Mifumo ya Usimamizi wa Kodi ya IDRAS na TANCIS ambayo inasomana na mifumo mingine ili kurahisisha zaidi ulipaji na ongezeko la Kodi.

5. Tunaweza kujenga Mifumo ya kusimamia Bandari zetu na mipaka yetu vizuri, na kuweka mazingira ya ushindani yaliyo sawa ili kuwezesha biashara na makusanyo ya kodi ya Forodha kuongezeka.

6. Tunaweza kuimarisha Huduma za Kodi pamoja na matumizi sahihi ya mfumo wa EFD na kuchukua hatua kwa wasiotumia kwa mujibu na kutumia Sheria za Kodi, mifumo ya usimamizi wa kodi( EFDMS) na ushirikiswaji wa walipakodi.

7. Tunaweza Kuendelea Kutoa Elimu ya Kodi kwa njia tofauti zenye tija na na zinazoleta matokeo chanya.

8. Tunaweza kuimarisha Ukaguzi na uchunguzi ili kuwatambua na kuwachukulia hatua wachache waepa na wakwepa kodi ili kuleta usawa katika shughuli za kiuchumi nchini.

9. Tunaweza kama TRA kuendelea kuongeza idadi ya walipakodi nchini, kuimarisha utoaji wa huduma nzuri, kuongeza Uweledi, Ubunifu na Uadilifu,pamoja na kuwajali wateja wetu ili kuimarisha ulipaji Kodi wa hiari nchini.

10. Tunaweza Kuendelea kushirikiana na wadau wote wa kodi, wakiwemo Viongozi wa taasisi na Jumuiya za Wafanyabiashara nchini ili kuendelea kujenga na kuimarisha Mfumo wa kodi ulio sawa, unao tabirika, unaowezesha ukuaji wa biashara nchini, wenye ufanisi, unaowezesha utatuzi wa migogoro ya kikodi kwa haraka na unaohamasisha wananchi na wafanyabiashara kufurahia kulipa kodi kwa hiari.

Nawashukuru sana walipakodi wote na kuwahakikishia, TRA, itaendelea kutekeleza Maagizo yote ya Mhe. Rais, ya kuwasikiliza walipakodi, Kuendelea Kutoa Elimu ya Kodi, kuweka Mazingira wezeshi ya shughuli za Kiuchumi nchini, Kuimarisha utoaji wa Huduma za Kodi na Kuendelea Kufanya vizuri zaidi ili kuiwezesha Serikali kutimiza Majukumu yake ya kuwaletea maendeleo wananchi.

KWA PAMOJA TUNAJENGA TAIFA LETU.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news