DAR-Matukio mbalimbali katika picha siku ya nne ya Kongamano la 8 la Mwaka la TEHAMA Tanzania kwa mwaka 2024 (8th Annual Tanzania ICT Conference) linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam Oktoba 16, 2024.
Kongamano hili ambalo limefunguliwa Oktoba 15,2024 na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa (Mb) lilianza Oktoba 13,2024 na linatarajiwa kufikia tamati Oktoba 17,2024.
Vilevile, kongamano hili linaongozwa na kauli mbiu isemayo Kutumia Uwezo wa Akili Mnemba na Roboti kwa Mapinduzi ya Kiuchumi na Kijamii. Kauli mbiu hiyo inafungua mjadala muhimu hususani kwa wakati huu ambapo Dunia nzima inashuhudia mapinduzi ya kidigitali.
Aidha, kesho Oktoba 17,2024 kongamano hilo linatarajiwa kufungwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa.