Simba Sports Club kufanya maboresho makubwa kidijitali

NA DIRAMAKINI

MWENYEKITI wa Klabu ya Simba (Simba Sports Club) ya jijini Dar es Salaam, Murtaza Mangungu amesema, klabu hiyo inaongeza njia za mawasiliano ili kuwafikia wanachama na wadau wake kila kona duniani.
"Tumezungumzia suala la digital platforms (kwenye bajeti ya 2024/2025 mitandao ya kijamii ya Simba inatarajiwa kuingiza shilingi milioni 400).

"Tuna mchakato unaoendelea, timu yetu inasafiri na kushiriki michuano mikubwa Afrika. Tunaanzisha chaneli kwa lugha ya Kiarabu na lugha ya Kifaransa."

Mangungu ameyasema hayo leo Oktoba 6,2024 katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Klabu ya Simba mwaka 2024.

Katika hatua nyingine, Mangungu amesema kuwa, “Sisi Bodi tutaunga utekelezaji wa mradi wa miundombinu, mwisho nitoe shukrani kwa Serikali, tunasafiri nchi mbalimbali na maafisa wa Ubalozi wamekuwa wakija tunashirikiana ili kila kitu kwenda vizuri.

"Sisi Simba Sports Club tutaendelea kuunga mkono Serikali, tunafikia hatua ya mwisho ya mabadiliko, lakini mabadiliko yoyote lazima yatakuwa na maumivu nadhani tuvumilie ili tumalize haya yote kwa pamoja.

“Tunamshukuru Rais wa Simba, Mohammed Dewji kwa hotuba nzuri, pamoja na kusisitiza wanachama na wapenzi wa Simba kwenda viwanjani kuiunga mkono timu yao.

"Kadhalika tunawasisitiza sana umuhimu wa kutumia bidhaa zinazotokana na wadhamini wetu,"amesisitiza Mangungu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news