Soma bure kurasa 54 za Diwani ya CHEZA NA AHADI ZAKO kutoka kwa Lwaga Mwambande

NA LWAGA MWAMBANDE

MPENDWA msomaji wangu, ninakusalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania popote ulipo...ninayo kila sababu ya kuedelea kumshukuru MUNGU wa Mbinguni kwa wema wake kila iitwapo leo katika maisha yangu na familia yangu.


Leo ni siku nyingine tena ambayo ninapenda kukushirikisha diwani yangu ya pili, ikiwa ni sehemu ya vitabu vitano ambavyo nilizindua Oktoba 17,2024 kupitia Moto Ulao Online Church (MUOC).

Aidha, leo ninakushirikisha Diwani ya CHEZA NA AHADI ZAKO. Huu ni mkusanyiko wa mashairi yanayoeleza umuhimu wa kuzingatia mambo yanayoweza kukuletea mafanikio katika maisha yako na kujiepusha na yale yanayoweza kukufanya ukapotea. Beti zinazopatikana katika diwani hii ni pamoja na:

Ee mtoto nakusihi, cheza na ahadi zako,
Ujihimu asubuhi, ufanye shughuli zako,
Wazazi na wafurahi, kwa huo mwenendo wako,
Uwaheshimu wazazi, uishi miaka mingi.


Bora kutotajirika, ubaki naye Rabuka,
Kuliko kutajirika, na Mungu akakutoka,
Huko ni kufilisika, na hakuna kuokoka,
Mwisho ni kuaibika, na kizazi kufutika.


Aidha, katika diwani hii ya CHEZA NA AHADI ZAKO, utajifunza Neno la Mungu kwa njia ya mashairi. Hivyo, utaimarishwa kimwili na kiroho. Utajisomea na kuimba beti kama hizi:

Upate talanta tano, upate talanta mbili,
Ile moja sema no! kwako isiwe halali,
Zile mbili nazo tano, zizalishe mara mbili,
Hata Mungu hupendezwa, tunapozaa matunda.


Ukiona wahalifu, ndio wanaoachiwa,
Na wale watakatifu, ndio wanaadhibiwa,
Hali isije kukifu, na Yesu alifanyiwa,
Haki uibondebonde, mwishowe inainuka.


Karibu ujisomee Cheza na Ahadi Zako, karibu ughani. Ya kuchukua, chukua; ya kuwagawia wengine wagawie. Ujengwe Imani yako iimarike. CHEZA NA AHADI ZAKO.

Bofya hapa kuisoma CHEZA NA AHADI ZAKO yote>>>

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news