Tanzania na Pakistan zakubaliana kupanua wigo wa ushirikiano

APIA-Tanzania na Pakistan zimekubaliana kupanua wigo wa ushirikiano ili kukuza uhusiano wa uwili baina ya nchi hizo mbili huku wakitilia maanani vipaumbele vya nchi zote mbili kwa manufaa ya nchi na wananchi wa pande zote mbili.
Wakizungumza pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) jijini Apia nchini Samoa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo pamoja na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan, Mhe. Muhammad Ishaq Dar wamekubaliana kuongeza ushirikiano katika kilimo, teknolojia, viwanda vya nguo na biashara.
Waziri Kombo ameishukuru Pakistan kwa ushirikiano mzuri uliopo kati yake na Tanzania kwa takribani miaka 60 sasa na kumpatia Mhe. Dar Kitabu picha cha ‘Photographic Journey: 60 Years of the United Republic of Tanzania’ kinachoonesha historia ya miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika picha ambapo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ameandika dibaji ya kitabu hicho.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news