DAR-Tanzania kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kushirikiana na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) imekuwa Mwenyeji wa mkutano wa Mafunzo ya WMO kwa wataalamu wa hali ya hewa kutoka nchi wanachama wa WMO Kanda ya Afrika Mashariki na Kaskazini.



Aidha, Jaji Mshibe ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuwekeza katika uboreshaji wa miundombinu ya huduma za hali ya hewa.
Jaji Mshibe amewashukuru pia WMO na washirika wengine kwa jitihada zao za kuimarisha huduma za hali ya hewa barani Afrika, ikiwemo kuanzisha mfuko wa uwezeshaji wa huduma za uangazi wa hali ya hewa.
Amesema, kupitia jitihada hizo, kiasi cha dola za kimarekani milioni 9 zimeidhinishwa kuboresha huduma za hali ya hewa nchini Tanzania.
Awali, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Mwakilishi wa Kudumu wa WMO, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi, Dkt. Ladislaus Chang’a ameeleza umuhimu wa kuimairsha uangazi na kuongeza upatakanaji wa data.

Ni kwa ajili ya kuimairsha utoaji wa tahadhari za matukio ya hali mbaya ya hewa na kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa.
Aidha,Dkt. Chang’a ameeleza kuwa,Tanzania kupitia TMA imejipanga kuendelea kushiriki katika kuongoza na kuwa kinara katika baadhi ya jitihada za kuimarisha huduma za hali ya hewa barani Afrika.
"Tumejiandaa vyema kuwa mwenyeji wa Mkutano huu mkubwa wa Kikanda, na pia kama mwenyeji wa Kituo cha mfumo wa Kidunia wa kufuatilia vituo vya uangazi wa hali ya hewa kwa nchi za Afrika Mashariki,” amesema Dkt. Chang’a.
TMA itawasilisha mada zenye kueleza uzoefu wake katika utekelezaji wa jukumu hilo.
Kwa upande wake, Mwakilishi kutoka WMO,Abubakari Salih Babiker amesema, kumekuwa na changamoto ya matukio mbalimbali ya hali mbaya ya hewa hivyo ushirikiano wetu utasaidia katka kutoa tahadhari za mapema juu ya matukio ya Hali mbaya ya Hewa na tahadhali za mapema,”amesema.

Tags
Habari
Kimataifa
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)
Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO)
Tanzania Meteorological Agency (TMA)