TEA yapitia na kutathmini mpango mkakati wake wa utekelezaji

NA MWANDISHI WETU

MENEJIMENTI ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Dkt. Erasmus Kipesha imekutana kwa siku mbili kuanzia Oktoba 21 na 22, 2024, kwa lengo la kutathmini utekelezaji wa majukumu yake kama yalivyoainishwa kwenye Mpango Mkakati wa miaka mitano (2021/2022 – 2025/2026).
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA),Dkt. Erasmus F. Kipesha akisisitiza jambo katika kikao maalumu cha Menejimenti cha kutathmini Mpango Mkakati wa Utekelezaji wa Mamlaka pamoja na majukumu yake.

Tathmini hiyo imelenga kubaini maeneo ya kuboresha na kuweka mikakati madhubuti ya kuimarisha ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya TEA.
Meneja Ufuatiliaji na Tathmini,Bi. Wendo Chiduo (Kulia) na Meneja Rasilimali Watu Bi. Alice Lukindo (Kushoto) wakifuatilia wasilisho la tathmini ya Mpango Mkakati wa TEA katika kikao maalumu cha Menejimenti kilichofanyika kwa lengo la kupitia mpango huo.
Kaimu Mkurugenzi Huduma za Taasisi, CPA Mwanahamis Chambega (Kulia) pamoja na Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA, Bw. Emmanuel Shirima wakifuatilia wasilisho la tathmini ya Mpango Mkakati wa TEA katika kikao maalumu cha Menejimenti kilichofanyika kwa lengo la kupitia Mpango huo.
Kaimu Mkurugenzi Utafutaji Rasilimali na Usimamizi wa Miradi,Bw. Masozi Nyirenda akifafanua jambo kuhusu Mpango wa Utekelezaji wa TEA pamoja na utekelezaji wa majukukumu ya Mamlaka hiyo.

Dkt. Kipesha, akizungumza na wajumbe wa Menejimenti, alisisitiza umuhimu wa kuhakikisha majukumu ya TEA yanaenda sanjari na utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014, ambayo inalenga kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kuwa bora, salama, na endelevu katika shule na vyuo.

Katika kikao hicho, wajumbe wa Menejimenti walipata fursa ya kujadili namna bora ya kusimamia na kutekeleza Mpango Mkakati huo katika kipindi kilichosalia cha miaka miwili, ili kuhakikisha malengo yote ya TEA yanafikiwa kwa ufanisi zaidi.
Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti wakifuatilia wasilisho la tathmini ya Mpango Mkakati wa TEA katika kikao maalumu kilichofanyika kwa lengo la kupitia Mpango huo.

Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ilianzishwa kupitia Sheria ya Bunge Na. 8 ya mwaka 2001, chini ya kifungu 5 (1), pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2013, kwa lengo la kuratibu uendeshaji wa Mfuko wa Elimu.

Lengo kuu la Mfuko wa Elimu ni kuimarisha juhudi za serikali katika kugharamia miradi ya elimu ili kuinua ubora na upatikanaji wake kwa usawa, katika ngazi zote za elimu kwa Tanzania Bara na elimu ya juu kwa Tanzania Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news