Tuendelee kujitathmini na kujua umuhimu wa ibada-Alhaj Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewasihi waumini wa dini ya Kiislamu kujitathmini na kujua umuhimu wa Ibada kwenye matendo yao ya kila siku.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhajj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na viongozi wa Masjid Fatma kwa Muhammed Ali Kidongochekundu Wilaya ya Mjini Unguja alipowasili kwa ajili ya Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika leo Oktoba 18,2024 katika msikiti huo.

Alhaj Dkt.Mwinyi ametoa nasaha hizo leo Oktoba 18,2024 alipotoa salamu kwa Waumini hao baada kujumuika nao kwenye ibada ya sala ya Ijumaa, msikiti wa Muhammad Ali, Kidongo Chekundu, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia waumini wa Dini ya Kiislamu baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid Fatma kwa Muhammed Ali Kidongochekundu Wilaya ya Mjini Unguja leo.

Pia,ameeleza kuwa, ni wajibu wa kila Muumini kuitathmini nafsi yake na anaowaongoza ili kubaini kiasi gani maisha yao yanalingana na Ibada wanazozitekeleza kila siku.
Waumini wa Dini ya Kiislamu wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na kuwasalimia baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid Fatma kwa Muhammed Ali Kidongochekundu Wilaya ya Mjini Unguja leo.

Amesema, kuna mambo mengi yanaendelea ndani ya jamii kwa sababu ya watu kukosa Ucha Mungu(taqwa).

Alhaj Dkt.Mwinyi ametaja baadhi ya mambo hayo kuwa ni pamoja na Udhalilishaji, ubakaji na wizi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsalimia Ndg. Salum Othman, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid Fatma kwa Muhammed Ali Kidongochekundu Wilaya ya Mjini Unguja leo.

Aidha, amewahimiza Waumini hao kufanya Ibada kwani Ndio sababu kuu ya kuumbwa kwao.

Akitoa Salamu Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Muft wa Zanzibar, Sheikh Khalid Ali Mfaume amewasisitiza viongozi kuwa mfano bora kwa watu wanaowaongoza kwa kutenda mambo mema.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsalimia Ndg. Salum Omar Khamis, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid Fatma kwa Muhammed Ali Kidongochekundu Wilaya ya Mjini Unguja leo.

Amewasisitiza Vijana kuacha kushawishika na kujiunga na makundi maovu kwa kisingizio cha dini badala yake kusimamisha sala kwa kuchunga wakati na nidhamu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news