Tume ya TEHAMA yakipeleka Kiswahili katika AI ya Waitaliano

DAR-Kampuni ya ALMAWAVE ya Italia imesaini Makubaliano ya Ushirikiano wa Kikazi (MoU) na Tume ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Tanzania (ICTC) kwa lengo la kuendeleza na kuingiza lugha ya Kiswahili katika programu yake Velvet ambayo ni mahsusi katika kukuza teknolojia ya Akili Mnemba (AI).
Makubaliano hayo yaliyofikiwa Oktoba 16, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa Kongamano la Nane la Mwaka la TEHAMA Tanzania yanalenga kuendeleza na kuanzisha mfano wa lugha wa Almawave (Velvet) katika toleo lake la Kiswahili ikiwa ni lugha rasmi ya Tanzania.

Aidha,ushirikiano huo utaweka mkazo katika kutoa mfumo wa Akili Mnemba ambao unaweza kutumika kwa ufanisi katika sekta za umma nchini Tanzania.

Kupitia, makubaliano hayo Almawave itatoa Velvet kama toleo la wazi kwa Tume ya TEHAMA, huku tume ikitoa taarifa (data) za ndani kwa ajili ya kufundisha mfano wa lugha ya Kiswahili.

Lengo ni kuunda mfano wa Modeli Kubwa ya Lugha (Large Language Model-LLM) ambao umejengwa kwa muktadha wa ndani, bila upendeleo na unaoweza kuboresha mchakato wa utawala kupitia digitali na kuongeza ufanisi wa huduma za umma na mawasiliano kwa wananchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Almawave,Valeria Sandei amesema kuwa,makubaliano hayo ni hatua muhimu katika safari yao ya ushirikiano na Tanzania na Bara la Afrika.

"Utekelezaji wa Velvet uliotengenezwa kwenye kompyuta yenye nguvu ya Leonardo unaonesha jinsi Akili Mnemba inavyoweza kuharakisha digitali na maendeleo ya kiuchumi.”

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA nchini,Dkt.Nkundwe Moses Mwasaga amebainisha kuwa, ushirikiano huu utaboresha uwezo wa kuendeleza ujuzi wa kitaaluma, kukusanya taarifa na kutekeleza miradi nchini.

"Tume ya TEHAMA ina jukumu muhimu la kuhamasisha uwekezaji katika Teknololojia ya Habari na Mawasiliano na kutoa ushauri kwa Serikali kuhusu masuala husika."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news