Tuwakatae wanasiasa na wanaharakati wachochezi kuelekea uchaguzi-Mchungaji Tengwa

NA GODFREY NNKO

MCHUNGAJI wa Kanisa la Uamsho na Matengenezo ya Kiroho Ulimwenguni, Mwalimu Augustine Tengwa amevishauri vyombo vya ulinzi na usalama kusimama vema katika nafasi zao ili kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaimarika zaidi kabla na baada ya chaguzi zijazo.
Ameyasema hayo leo Oktoba 11,2024 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo ameangazia umuhimu wa maombi ya kuliombea Taifa kuelekea uchaguzi.

Mchungaji Tengwa akiwa ameambatana na wachungaji wasaidizi katika huduma hiyo yenye makao makuu mkoani Morogoro amesema, kupitia maombi ambayo wamekuwa wakiyafanya mfululizo, Mungu amewaonesha ishara ambayo si njema katika chaguzi zijazo nchini.
Amesema, kutokana na hali hiyo kila Mtanzania analo jukumu la kuhakikisha amani ya nchi inatawala na wanapaswa kuwakemea ikiwemo kuwakataa watu au wanasiasa wachochezi.

Tengwa amesema, Tanzania ni ya Watanzania na hawana taifa mbadala la kukimbilia iwapo wataruhusu wenye nia ovu kutimiza matakwa yao ili kupata nafasi za uongozi.
Kwa upande wake, Nabii Alpha Kiamba amewataka Watanzania kuyapa kisogo maneno na taarifa zenye viashiria vya kuwagawa ambavyo vimekuwa vikizushwa na baadhi ya wanasiasa wakiwemo wanaharakati mbalimbali.

"Na, suala la upinzani nchini lifanyike katika hekima za Mungu, kwani taarifa zinatolewa ili kuliokoa Taifa na mauti.

"Ndiyo maana tutahitaji watu waombe, kila mkoa watu waingie kwenye maombi.Sasa Mama naye mnampiga mawe usiku na mchana.Watu wanaokutana na vyombo vya dola na viongozi wakuu wawe na hekima za kushauri."

"Sisi kama watumishi wa Mungu ni mabalozi wa Mungu."

Amesema, mara nyingi wamekuwa wakifanya maombi na wanaamini Tanzania bila maombi hakuna taifa.

"Tumekuwa na kasumba fulani ya kupuuza taarifa kwa kuwa eti inatoka Mbinguni...ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.

"Kila mtu anapaswa kusimama katika nafasi yake."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news