Tuwapinge wote wasioitakia mema Tanzania kuelekea uchaguzi-IJP Wambura

KILIMANJARO-Jeshi la Polisi nchini limesema katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwakani, halitavumilia mtu au kikundi cha watu kitakachovunja sheria kwa kisingizio chochote.

Pia,limesema hatua za kisheria zitachukuliwa, ili jamii iendelee kuishi kwa amani na kutimiza haki ya kikatiba kushiriki uchaguzi huo.
Mkuu wa Jeshi hilo, Inspekta Jenerali wa Polisi, IJP Camilus Wambura ameyasema hayo wakati akifunga Mafunzo ya Awali ya Polisi Kozi Namba Moja ya Mwaka 2023/24 yaliyofanyika katika Shule ya Polisi Tanzania (CCP), Moshi mkoani Kilimanjaro.

IJP Wambura alisema, Jeshi la Polisi pamoja na kutekeleza majukumu yake, lina wajibu wa kuhakikisha amani na utulivu vinatamalaki na askari wote wanadumisha amani na uzalendo kwa taifa, kwa kusimamia sheria na kanuni za uchaguzi.

“Tuwapinge wote wenye nia mbaya wasioitakia mema Tanzania. Tuwapinge wote wenye nia mbaya wanaoshabikia uhalifu au vitendo vya uvunjifu wa amani ambavyo vingi vinachochewa na itikadi za siasa chafu, kwa maslahi ya watu wachache."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news