WASHINGTON D.C-Ujumbe wa Tanzania, ukiongozwa na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba, umekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF), anayesimamia Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika (Africa Group 1 Constituency), Bw. Willie Nakuyanda. Katika ujumbe huo, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, alikuwepo pia.
Katika kikao hicho, Bw. Nakuyanda aliipongeza Tanzania kwa usimamizi bora wa uchumi, akisisitiza mafanikio ya programu ya "Extended Credit Facility" ambayo Tanzania inanufaika nayo kupitia IMF.