VIDEO:Rais Dkt.Samia awapa furaha wakulima wa korosho kilo moja yafika shilingi 4,120

MTWARA-Mnada wa kwanza wa korosho kwa msimu wa 2024-2025 umefanyika kupitia Chama Kikuu cha Ushirika cha TANECU kinachohudumia Wilaya ya Tandahimba na Newala mkoani Mtwara.
Jumla ya tani 3,857 za korosho ghafi ziliuzwa kwa kutumia mfumo wa soko la bidhaa Tanzania (TMX) Bei ya juu iliyofikiwa ni shilingi 4120 kwa kilo na bei ya chini ni shilingi 4,035 kwa kilo kutoka bei ya shilingi 2500 kwa kilo.

Wakulima wa kutoka Tandahimba na Newala wanaishukuru serikali ya Rais Samia kwa kusikia kilio chao kwa bei nzuri ambayo haijawahi kutokea kwani kwa miaka kadhaa nyuma bei haikuwa nzuri.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news