"Kuhusiana na dawa za kulevya, kwa uelewa wangu mimi, ninaweza nikaelezea kwa sehemu na baadhi ya sehemu kwa sababu niliwahi kutumia kwa muda wa miaka kama 10, lakini mimi nilitumia bangi.
"Ninavyoweza kuelezea, kitu cha kwanza unapotumia yanakufanya uridhike,ile hali uliyonayo uridhike nayo,mfano kipindi nikitumia bangi, mimi nilikuwa nikikosa kazi.
"Nikishavuta basi, kitu ninachosema yupo Mungu na ninajua kesho ninapata, kwa hiyo inakufanya uridhike na ukubaliane na mazingira yale.
"Bila ya kujua kwamba, pamoja na kwamba nimekosa nina hatua ninatakiwa nichukue, nifuatilie na ninaweza nikapata shughuli, kwa kweli Serikali iweke nguvu katika hili.
"Na niiombe sana, ijitahidi kuangalia mtandao huu kwa sababu wamekuwa wakishikwa watumiaji, wakishikwa na hata wanaowauzia, lakini ninajua wapo mabwana wanaowatuma na wanaowapa hao wanaowauzia hao wadogo.
"Niombe adhabu ingewekwa kubwa kwa hawa watu ambao wanatoa mizigo nje ya nchi,na kuileta ndani na kuisambaza kwa mawakala, la kuwashauri vijana wenzangu ni kwamba, madawa (dawa za) kulevya hayafai,na usijiingize wala usiseme unajaribu kwa sababu mimi kuingia ilikuwa ni kama ninajaribu.
"Kwa sababu mtaa nilioishi tulikuwa vijana wengi, na katika kutotumia kulikuwa na kauli ambayo ilikuwa inatumika kwamba usipotumia, usipofanya mambo ya kihuni, unaitwa mtoto wa mama.
"Kwa hiyo, na mimi ile sifa nikataka niikatae, ili kuwaridhisha vijana wenzangu ikabidi niingie,"Frank Charles Dida ambaye ambaye amewahi kuwa mraibu wa bangi kwa miaka 10 amebainisha;
Tags
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Kataa Dawa za Kulevya na Timiza Ndoto Zako
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)