Viongozi na wananchi wamiminika banda la BoT maonesho ya Saba ya Teknolojia ya Madini mjini Geita

GEITA-Viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wameendelea kutembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenye Maonesho ya Saba ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya Bombambili mkoani Geita. 

Miongoni mwa viongozi hao ni pamoja na Waziri wa Madini, Mhe. Anothny Mavunde na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Martine Shigela.
Katika Maonesho hayo Benki Kuu inatoa elimu kwa umma kuhusu majukumu yake katika kusimamia ustawi wa Uchumi na maendeleo ya sekta ya fedha nchini.
Vilevile, wananchi wanaotembelea banda letu wanapata fursa ya kufahamu zaidi kuhusu mpango wa ununuzi wa dhahabu nchini wenye lengo la kuongeza akiba ya nchi ya fedha za kigeni na kuimarisha thamani ya shilingi yetu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news