Waajiri wasiotekeleza Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi watajwa kuwa kikwazo

NA MARY GWERA
Mahakama Arusha

BAADHI ya Waajiri wasiotekeleza Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi wametajwa kukwamisha jitihada za Serikali za kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanakuwa na uhakika wa kipato pale wanapopata ulemavu kutokana na ajali au magonjwa wanayopata katika utekelezaji wa majukumu yao ya kikazi na iwapo watafariki kutokana na ajali au magonjwa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb) akizungumza leo tarehe 08 Oktoba, 2024 wakati wa akifunga Kikao Kazi kati ya Majaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania na Menejimenti ya Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF) katika Hoteli ya 'Mount' Meru jijini Arusha.

Hayo yamebainishwa leo tarehe 08 Oktoba, 2024 mkoani Arusha na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb) wakati wa akifunga Kikao Kazi kati ya Majaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania na Menejimenti ya Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb) akizungumza leo tarehe 08 Oktoba, 2024 wakati wa akifunga Kikao Kazi kati ya Majaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania na Menejimenti ya Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF) katika Hoteli ya 'Mount' Meru jijini Arusha.

“Eneo ambalo tunatamani zaidi kuendelea kupata mapendekezo yenu Waheshimiwa ni juu ya namna gani rahisi ya kuwashughulikia waajiri ambao hawajajisajili WCF na ambao hawawasilishi michango ya wafanyakazi wao kwa wakati, eneo hili ni muhimu sana,” amesema Mhe. Kikwete.

Waziri Kikwete amesema, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua na kuthamini mchango wa wafanyakazi katika sekta zote na ndio maana imeendelea kutekeleza na kuboresha sheria za hifadhi ya jamii.
Meza kuu ikiongozwa na Mgeni Rasmi ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb) (katikati) katika picha ya pamoja na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha, Mhe. Ilvin Mugeta (wa kwanza kushoto), Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, Mhe. Dkt. Yose Mlyambina (wa pili kushoto), Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Victor Kategere (wa kwanza kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma (wa pili kulia).

“Katika kipindi kifupi cha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita tumeshuhudia mabadiliko mbalimbali katika sekta ya hifadhi ya jamii. Moja ya maboresho hayo makubwa ni kupunguza kiwango cha uchangiaji kwa waajiri wa sekta binafsi kwa WCF kutoka asilimia moja ya mshahara wa mfanyakazi kila mwezi hadi kufikia asilimia 0.5,” amesema Waziri huyo.
Sehemu ya Majaji wa Mahakama ya Rufani wakifuatilia hotuba ya kufunga Kikao Kazi kati ya Majaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania na Menejimenti ya Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF) iliyokuwa ikitolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb) (hayupo katika picha) katika Hoteli ya 'Mount' Meru jijini Arusha.

Amesema kuwa, maboresho mengine ni kupunguza kiwango cha riba kutoka asilimia 10 hadi asilimia mbili kwa mwezi kwa waajiri wanaochelewa kuwasilisha michango ya kila mwezi ya wafanyakazi wao na kwamba Serikali kupitia WCF imeongeza kiwango cha chini cha mshahara unaotumika kukokotoa fidia hadi kufikia shilingi 393,861.19 kwa mwezi, ikiwa ni uwezeshaji mkubwa wa kipato kwa watumishi wenye viwango vidogo vya mshahara.

Akizungumzia kuhusu kikao kazi hicho kilichowashirikisha Majaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Kikwete amesema kwamba maoni yote yaliyopokelewa yatachukuliwa kwa uzito kama ilivyokuwa katika vikao kazi vilivyopita.

“Mathalani, maoni yaliyotolewa katika vikao vilivyotangulia ya kuboresha kifungu cha 39 (2) cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi [Sura 263] kilichoweka ukomo wa muda wa kuwasilisha madai bila kutoa wigo wa kupokea madai hayo iwapo kuna sababu za msingi za kucheleweshwa kwake, tumeshayafanyia kazi. Maboresho ya kifungu hicho yameshapitishwa na Bunge tarehe 29 Agosti, 2024 katika Muswada wa Marekebisho ya Sheria za Hifadhi ya Jamii,” ameeleza Waziri huyo.

Ameongeza kuwa, wakati anawasilisha Muswada huo bungeni alieleza kuwa, dhumuni kubwa ni kuboresha utoaji haki kwa wafanyakazi wanaoumia kazini na kuondoa vikwazo vinavyopelekea wafanyakazi hao kukosa fidia pale ambapo kuna sababu za msingi za kushindwa kutoa taarifa ndani ya muda wa kisheria.
Meza kuu katika picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama ya Rufani (waliosimama nyuma). Walioketi katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb), Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha, Mhe. Ilvin Mugeta (wa kwanza kushoto), Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, Mhe. Dkt. Yose Mlyambina (wa pili kushoto), Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Victor Kategere (wa kwanza kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma (wa pili kulia).
Meza kuu katika picha ya pamoja na mmoja wa Sekreatrieti ya maandalizi ya kikao hicho ambaye ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, Mhe. Biswalo Mganga (aliyesimama nyuma).
Meza Kuu katika picha za pamoja na Naibu Wasajili wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu ya Tanzania.

Amewashukuru Majaji wa Mahakama ya Rufani kwa kukubali kushiriki katika kikao kazi hicho licha ya kuwa na ratiba ngumu katika kutekeleza majukumu yao, ambapo amesema, “hakika uwepo wenu hapa kama washiriki unadhihirisha umuhimu wa ushirikiano kwa Mahakama na Serikali kupitia WCF katika kuwahudumia Watanzania na kuhakikisha kuwa Sheria za Kazi, hususani Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi [Sura 263], zinatekelezwa kwa ufanisi na kwa haki.”

Akitoa neno la utangulizi kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Bw. Victor Kategere ameushukuru Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa namna ambavyo wameendelea kukubali maombi yetu ya kuwezesha vikao kazi mbalimbali vilivyofanyika nchi nzima ambavyo vimewajengea uwezo watendaji wa Mahakama katika ngazi mbalimbali wameweza kujadili kwa pamoja Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi (Sura 263) kwa lengo la kuboresha mahusiano yaliyopo kati ya Mwajiri na Mwajiriwa.

“Kwa niaba ya Uongozi wa Mahakama ninaomba mpokee shukrani zetu za dhati.Kwa kumbukumbu zilizopo hiki ni kikao kazi hiki ni cha saba kikitanguliwa na vikao sita vilifanyika katika maeneo mbalimbali nchini; Bagamoyo, Mwanza, Arusha, Songea, Kigoma na Zanzibar,” amesema Bw. Kategere.

Mtendaji huyo amesema kufanyika kwa mafunzo hayo ni mwendelezo wa jitihada za kufanikisha Mpango Mkakati wa Mahakama (2020/2021 -2024/2025) katika utekelezaji wa nguzo ya pili ya ‘‘Upatikanaji Haki kwa Wakati’’ na kwamba ana imani kuwa, maarifa na ujuzi waliopata kupitia mafunzo hayo yatawasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao ya kazi.
Meza kuu ikiongozwa na Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb) (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya watumishi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).
Meza Kuu na Wawezeshaji waliotoa mada mbalimbali katika Kikao Kazi kati ya Mahakama ya Rufani na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).
Meza Kuu na Wadau wa Kazi.
Meza kuu katika picha ya pamoja na Kaimu Mtendaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Bw. Jumanne Msuta (aliyesimama kulia) pamoja na Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Mahakama ya Tanzania, Stephen Magoha (kushoto).
Meza Kuu katika picha ya pamoja na Kamati ya Maandalizi ya kikao hicho.
Meza kuu ikiongozwa na Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb) (katikati) ikiwa pamoja na Mnufaika wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) alipata ajali akiwa kazini.
Waziri Kikwete (kulia) akiteta jambo na Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi (kushoto).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb) (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya Majaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mahakama na Mkurugenzi Mkuu wa WCF.(NA MARY GWERA, Mahakama).

“Aidha, katika kuifanikisha nguzo namba tatu ya Mpango Mkakati huo ya ‘‘urejeshwaji wa imani kwa wananchi na ushirikishwaji wa wadau,’’ ambalo kwa hili tunapenda kuushukuru Mhimili wa Serikali chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ambapo kwa jitihada zake ameiwezesha Mahakama kufanikisha malengo na mipango yake kwa kupitia wadau mbalimbali ikiwa pamoja na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ambao ndio wawezeshaji wa vikao kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na hiki,” amesema.

Kupitia kikao kazi hicho cha siku mbili (2) kilichofanyika tarehe 7 na 8 Oktoba mwaka huu, Majaji wa Mahakama ya Rufani wamepata uelewa jinsi Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) unavyofanya kazi pamoja na manufaa yake. Kadhalika wamepata fursa ya kutoa maoni yao kuhusu maboresho ya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi [Sura 263] ambayo WCF wameyachukua na kuahidi kuyafanyia kazi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news