Wafanya mazungumzo na Sekretarieti ya Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya Nne nchini Tanzania

DAR-Ujumbe kutoka Baraza la Michezo la Umoja Afrika pamoja na wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Sekretarieti ya Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya Nne leo Oktoba 15, 2024 jijini Dar es Salaam, umetembelea na kufanya mazungumzo na Sekretarieti ya Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya Nne.Baraza hilo makao makuu yake yapo hapa nchini Tanzania jijini Dodoma kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa majukumu ya sekretarieti hiyo kwa mafanikio ya sekta hiyo katika ukanda huo.
Kanda ya nne ya kimichezo kwa Afrika inajumuisha nchi 14 ikiwemo Makao Makuu Tanzania, Comoros, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Madagascar, Mauritius, Rwanda, Seychelles, Somalia, South Sudan, Sudan, na Uganda.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news