MBEYA-Wanafunzi kutoka Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Mbeya, wametembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayofanyika katika uwanja wa Ruanda Nzovwe jijini Mbeya, kuanzia tarehe 21 hadi 26 Oktoba 2024.