Wanaharakati wanaomchafua Rais Samia waumbuka

NAIROBI-Taasisi moja inayohusishwa na baadhi ya wanaharakati waliojificha Nairobi inadai CCM Tanzania imenunua haya magari kwa bei ya $200,000 (TZS 540,000).

Uki-search Google kwa haraka haraka tu, utagundua picha zilizo postiwa kwenye ukurasa wa taasisi hiyo zinatoka kwenye makala ya BBC Top Gear yenye kichwa cha habari "This Secret Dealer Is Selling New Old Toyota Land Cruisers That Are Supposed To Save The World."

Uzushi wenyewe.

Picha hiyo inayodaiwa na taasisi hiyo kuwa imepigwa picha kwenye eneo la chini la kuegesha magari ya UVCCM pale Lumumba kiuhalisia ni picha ya Toyota 650 ambazo zipo kwenye stoo moja nchini Uholanzi zikisubiria wateja.

Genge hili limekuwa likimchafua Mhe. Rais kwa mambo ya uongo na uzushi pamoja na familia yake na watu wake wa karibu.

Tulijua genge hilo limeishiwa hoja kwa muda mrefu ila hatukujua wameishiwa kiasi hichi.

Sasa hivi wanaishia kutunga hadithi kila leo ambazo hazina ukweli kwa lengo la kuendeleza ajenda zao.
Picha zilizookotwa mitandaoni.

Ila hatushangai. Tunajua bila ajenda hizi Mwanaharakati huyo anayeishi Nairobi atakosa hela za wafadhili na hela za kuwalipa posho vijana wake amaowatumia kusambaza ajenda zake.

Ni wakati sasa Mwanaharakati huyu atumie kipaji chake cha kutengeneza uongo aanze kutunga script za tamthilia ili alipwe kuweka hadithi zake kwenye luninga.

Hakika Mwanaharakati huyu ni director wa uongo na Mariawood ndio kiwanda cha kutengeneza uongo huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news