SINGIDA-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) leo Oktoba 15, 2024 amejiandikisha katika daftari la wapiga kura wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kituo cha Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji cha Misigiri kilichopo Kata ya Ulemo wilayani Iramba, mkoani Singida.

Akizungumza na wananchi hao ametoa rai kwa wananchi kutambua kuwa uandikishaji wa daftari la kudumu la uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Septemba mwaka huu, haumpi sifa mwananchi kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa isipokuwa hadi ajiandikishe kwenye daftari litakalomwezesha kuwachagua viongozi anaowataka katika ngazi ya Serikali za Mitaa.

“Napenda kutoa wito kwa wananchi kuwa mjitokeze kujiandikisha kwani zoezi halitumii muda mrefu, ndani ya dakika moja unakuwa umemaliza kujiandikisha,” amesema Dkt. Nchemba.