Waziri Balozi Dkt.Chana awasili Rukwa kwa ziara ya kikazi

RUKWA-Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amewasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo leo Oktoba 1,2024.
Mhe. Chana amefanya kikao na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa, Msalika Makungu, Mkuu wa Wilaya Sumbawanga, Nyakia Chirukile na baadhi ya Maafisa ya Waandamizi wa Mkoa wa Rukwa ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza juu ya umuhimu wa kuelimisha wananchi kuacha kuanzisha moto kwenye misitu, kupanda miti pamoja na kuainisha maeneo ya wananchi yenye changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu kwa ajili ya kuwavuna.
Aidha, Mhe. Chana amesema changamoto zote zinazoihusu sekta ya Maliasili na Utalii zitafanyiwa kazi huku akisisitiza wananchi wanaojishughulisha na shughuli za ufugaji nyuki ni lazima wapewe elimu ya kutumia mizinga ya kisasa ili waweze kuzalisha asali kwa kiwango kikubwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news