Waziri Dkt.Nchemba afanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia jijini Dodoma

DODOMA-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amekutana na kufanya Mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Bi. Victoria Kwakwa, baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara ya Fedha jijini Dodoma. Bi. Kwakwa yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Benki ya Dunia.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Bi. Victoria Kwakwa (kushoto), akizungumza jambo na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ambaye pia ni Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, katika ofisi ya Mhe. Waziri, Jijini Dodoma. Bi. Kwakwa yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akimkaribisha Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Bi. Victoria Kwakwa, baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara ya Fedha jijini Dodoma. Bi. Kwakwa yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Bi. Victoria Kwakwa, Ofisini Kwake Jijini Dodoma. Bi. Kwakwa yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Waziri wa Fedha, Mhe, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiongozana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Bi. Victoria Kwakwa, baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara ya Fedha-Treasury Squire jijini Dodoma, akiwa katika ziara ya kikazi ya siku tatu nchini Tanzania, ambapo walijadiliana masuala kadhaa ya ushirikiano kati ya Tanzania na Benki ya Dunia.
Waziri wa Fedha, Mhe, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiagana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Bi. Victoria Kwakwa, baada ya kikao kati yao kilichofanyika jijini Dodoma. Bi. Kwakwa yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha -Dodoma).

Bi. Kwakwa alilakiwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Naibu Katibu Mkuu, Bw. Elijah Mwandumbya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news